Post Your Ad

Mpangaji Bidhaa na Mtoa huduma kwa Wateja – Supermarket

TZS 0

Product Details:

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Nafasi: Mpangaji Bidhaa na Mtoa huduma kwa Wateja – Supermarket - Kigamboni Muda wa Kazi: Wiki Mshahara: Maelewano. Majukumu Makuu: • Kupanga bidhaa kwenye rafu kwa mpangilio unaovutia, unaofuata tarehe za mwisho wa matumizi, na unaorahisisha upatikanaji kwa wateja. • Kudumisha usafi na mpangilio wa eneo la bidhaa dukani. • Kukagua bidhaa mara kwa mara na kutoa taarifa kwa usimamizi kuhusu bidhaa zilizoharibika au zinazohitaji kuagizwa upya. • Kuwasaidia wateja kwa kuwapatia maelekezo ya bidhaa, mahali zilipo, na taarifa nyingine muhimu. • Kutoa huduma bora kwa wateja kwa lugha ya staha, tabasamu, na kwa moyo wa kusaidia. • Kushiriki katika shughuli za kufunga duka ikiwemo kupanga bidhaa, usafi wa mwisho wa siku na maandalizi ya siku inayofuata. • Kukusanya maoni ya wateja na kuyawasilisha kwa wasimamizi pale inapohitajika. Sifa za Mwombaji: • Awe na elimu ya angalau kuanzia kidato cha sita ( form Six) au cha nne (Form Four). • Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wateja kwa Kiswahili fasaha na Kiingereza ni ziada). • Awe mnyenyekevu, mchangamfu, na mwenye moyo wa kuhudumia watu. • Uzoefu wa kazi kwenye supermarket au sehemu ya rejareja utapewa kipaumbele. • Awe tayari kufanya kazi kwa zamu, pamoja na siku za mwisho wa wiki na sikukuu. Jinsi ya Kuomba: Tuma maombi yako (barua ya maombi na wasifu binafsi kupitia WhatsApp. Tafadhali usipige simu mawasiliano yote yatafanyika kupitia WhatsApp. Muda wa mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 12/7/2025