Hizi ni sub meter maalum ambazo zimefungwa rilei (Relay- hiki ni kifaa cha umeme kinacho fanya kazi kama switch) amabayo inakuwezesha kutumia kama luku ya tanesco ya kawaida ila hii inafanya kazi pamoja na luku ya tanesco
UFANYAJI KAZI WAKE
Aina tofauti na luku ya tanesco kama nilivosema ila hii inafanya kazi na luku ya tanesco kama meter kuu
Kwa mfano
Nina wapangaji wa 4 kwenye nyumba moja na tunatumia LUKU MOJA YA TANESCO
Kinacho fanyika kama kwa kila chumba nikafunga sub meter ya kutumia unit. Kama kwenye LUKU KUNA UNIT 40 mnao uwezo wa kugawana uni 10 kila mmoja
Na ikitokea katika mgawanyo huo wa unit kuna mmoja ametumia zake zimeisha bc umeme unakata kwake tu pasipo kuwa buguz watumiaji wengine na ikitokea anaitaji umeme italazimika aweke kwenye luku kubwa ili aweze kupata halali ya unit zake alizo weka tena (ata kawiwa kwa kiasi alichoongeza)
UGAWAJI WA UNIT
KATIKA HIZI sub meter TUNAPOKUFUNGIA LAZIMA UPEWE ACCOUNT AMBAYO IKO KATIKA MFUMO WA WEBSITE yaa ni utapewa USER NAME NA PASSWORD ambayo hyo account itakuwezesha kugawa unit katika hizi sub meter zingine ambazo ziko katika link (zilizo unganishwa na hyo luku) inamaana utakapo weka umeme kwenye luku ya tanesco ili ugawiwe unit zako ni lazima mtu alie kabiziwa hii account aingie na achague kiasi cha unit ulizo weka katika luku ya tanesco akisha chagua ile account itakupa token ambazo utaingiza katika sub meter yako na utakua unatumia umeme ulio lipia.